JANET JACKSON USO KWA USO NA MTALAKA WAKE

MARA baada ya kitambo cha zaidi ya miezi minne kupita bila ya kuonana na mzazi mwenzake, Janet Jackson pamoja na bilionea Wissam Al Mana wamekutana mahakamani kusikiliza shauri lao la madai ya talaka.

Janet pamoja na Al Mana wameonekana pamoja wiki iliyopita kwa mara ya kwanza tangu Aprili katika mahakama ya Royal Courts of Justice, jijini London ambako ndiko shauri lao linakosikilizwa.

Mwanamama huyo anayetamba na vibao vikali kama vile “Come Back to Me”, “Burn It Up”, “Together Again” na vingine vingi, ameamua kudai talaka hiyo kutokana na mumewe kuwa bize na mambo yake.


Janet aliolewa na bilionea Wissam mwaka 2012 na katika ndoa hiyo wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Eissa al Mana, ambaye amezaliwa Januari, mwaka huu na baada ya kuzaliwa mtoto huyo wawili hao walitengana.

No comments