JE, UNAJUA? ALEXIS SANCHEZ AMEKUBALI KUJIUNMGA MANCHESTER CITY

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza, Alexis Sanchez anatajwa kuwa amekubali kujiunga na klabu ya Manchester City.

Mwandishi mmoja wa habari ambaye ni rafiki mkubwa wa mwanasoka huyo amesema jana kwamba ameambiwa “laivu” na Sanchez kwamba anaondoka rasmi na chaguo lake ni Manchester City.    

 Gerard Romero ambaye ni mwandishi wa habari raia wa Hispania amesema kwamba ameambiwa na sanchez kwamba anakwenda Man City ili kuungana na kocha wakw wa zamani Pep Guardiola.

Arsenal imekuwa kwa muda mrefu sasa ikihaha kumbakiza mchezaji huyo katika kikosi chake, lakini kwa tarifa hizo mpya ni kama vile jitihada hizo zimekwama.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na msimu bora katika Arsenal chini ya kocha wake, Arsene Wenger na ametumbukiza kambani mabao 30 katika mechi zote za mashindano.

Hata hivyo, winga huyo yuko nje ya mkataba msimu ujao na kama anaondoka kwenda Man City maana yake anaondoka akiwa kama mchezaji huru.

Na kwa mujibu wa Romero, tayari mazungumzo ya uhamisho wake yanaweza kuanza wakati wowote ili kujua ni kiasi gani arsenal inaweza kumpa kutokana na muda mdogo wa mkataba wake uliobaki.

Mwandishi huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Alexis Sanchez amekamilisha uhamisho wake kwenda man City. Manchester na Arsenal wameridhia uhamisho wake.”

Wiki iliyopita Sanchez ameiambia Arsenal kwamba hana haraka ya kujadili kuhusu mkataba mpya mpaka baada ya mashindano ya Kombe la mabara.


Pep Guardiola amekuwa katika mawindo makali ya kusaka wachezaji wa maana kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.

No comments