JINA LA MLINZI WA BAYER LEVERKUSEN MEZANI KWA TOTTENHAM

TOTTENHAM Hotspur wameweka jina la mlinzi wa Bayer Leverkusen, Robert Hilbert.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Spur inapambana na klabu nyingine zinazowania saini ya mlinzi huyo zikiwemo klabu nyingi za Ulaya, zikiwemo Nice, Torino na westham United.

Robert Hilbert amekuwa katika kiwango kizuri kwa miaka miwili iliyopita na kuwa tegemeo katika kikosi cha Bayer Leverkusen.

Mlinzi huyo amekuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kuingia katika rada za usajili wa Spur inayopanga kupambana kwa ajili ya kumaliza ikiwa katika orodha ya timu nne za juu katika Ligi ya premier msimu huu.


Mawakala wa Tottenham wamekuwa wakisafiri mara kwa mara hadi nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiridhisha na kiwango cha sasa cha mlinzi huyo.

No comments