JOKATE SASA KUANZISHA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIPODOZI

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo “Kidoti” amesema kuwa kwa hivi sasa yuko kwenye mkakati wa kumiliki kiwanda kitakachokuwa kinazalisha vipodozi vya wanawake hapa nchini.

Staa huyo ambaye alisisitiza kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kama nguzo ya mafanikio yake kiuchumi, aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ambayo inaingiza vipodozi vingi kwa gharama kubwa hivyo anaona ni fursa kwake ya kufanya biashara hiyo.

“Nahisi nitakuwa mwanamitindo kamili kwa kumiliki kiwanda cha kuzalisha vipodozi hapa nchini na kupunguza uingizwaji wake,” alisema Jokate.

“Nimekuwa makini sana katika utafutaji wangu lakini pia nina nidhamu ya matumizi ya fedha ndio maana nafanikiwa kiuchumi,” aliongeza sta huyo.


Jokate nimrembo pekee aliyetajwa na jarida la Forbes hapa nchini baada ya kupata mafanikio makubwa kupitia biashara ya nywele.

No comments