JOSE MLOURINHO AANIKA SABABU YA KUMNG'OA VICTOR LINDELOF BENFICA... awaponda "kiaina" Blind na Bailly

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho ameeleza sababu ya kuvunja benki na kumnyakua mlinzi kinda wa klabu ya Benfica, Victor Lindelof na kusema ni kutokana na kutaka kukamilisha malengo ya kuwa na ukuta imara.

Kisha Mourinho alimweka katika imani kubwa Lindelof na kumfananisha na aliyewahi kuwa beki kisiki wa United, Rio Ferdnand.

Usajili wa Victor Lindelof mwenye umri wa miaka 22 umeigharimu Manchester United kiasi cha euro mil 30.7 kama hatua ya kuimarisha kikosi cha msimum ujao cha mashetani wekundu hao wa Old Trafford.

Akinukuliwa na Sky Sports, Mourinho alisema: “Kufanikiwa kumsajili Lindelof ni hatua kubwa ndani ya United kwani ni mpango endelevu wa kuimarisha idara ya ulinzi.”

“Kwa miaka mingi United imekosa walinzi wa sifa kama Rio Fernand, hivyo ninaamini huyu Lindelof ni kama ana vigezo vitakavyomfikisha katika kiwango cha beki huyo wa zamani.”

“Alikuwa katika mipango yangu ya miaka mingi kwasababu ninamfahamu na nimekuwa nikimfuatilia kwa ajili ya United. Ninaamini katika kila jambo kuhusu mlinzi huyu,” amesisitia Mourinho.  

Usajili wa Lindelof unaifanya idara ya ulinzi ya United kuwa kamili, ikiwa pia na Eric Bailly na Dalley Blind.

Lakini maelezo ya awali ya Mourinho aliwazungumzia Blind na Bailly kama aina ya walinzi wanaojua tu kukaba lakini wanakosa sifa ya kumalizia kazi ya mwisho ambayo ni kutoa pasi ya uhakika, sifa ambayo Lindelof anayo.  


Jarida moja nchini Ureno limeandika kuhusu mashabiki wa Benfica waliomwelezea Lendelof kama ni kati ya walinzi bora zaidi duniani, hivto United ni kama wamelamba dume.

No comments