JUAN MATA AFANIKIWA KUMALIZA “TIFU LAKE” NA KOCHA JOSE MOURINHO

KAMA unadhani lile bifu baina ya bosi wa Manchester United, Jose Mourinho na Juan Mata linaendelea, itabidi usikilizie kwanza.

Kwani mambo yanayoendelea hivi sasa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu ni kama vile Juan Mata amefanikiwa kubadilisha akili za kocha wake huyo.

Hatua hiyo inafuatia ukweli kuwa kocha Jose Mourinho ameonyesha dalili zote za kumbakiza mchezaji huyo katika kikosi cha msimu ujao.

Mourinho hakuwa na uhusiano mzuri na Mata tangu walipokutana wakiwa Chelsea, kiasi cha kufikia hatua ya kumuuza straika huyo Manchester United ambako wamekutana tena.

Akinukuliwa, Mourinho alisema: “Jambo moja huweza kuandika historia mpya hasa katika matukio ya kweli tena hadharani.”

“Watu wanadai mambo yaliyopita katika klabu nyingine yangeweza kujitokeza pia hapa. Hivyo ni tofauti kabisa,” amenukuliwa Mourinho akiliambia ESPN.

“Ninamuamini Mata kama sehemu ya wachezaji wangu katika kikosi change cha msimu ujao.”


“Atabaki hapa kwa kipindi kirefu kuliko watu wanavyodhani. Huyu ni mchezaji anayeweza kubadilisha matokeo wakati wowote,” alisisitiza Mourinho.

No comments