JUVENTUS YAJIPANGA KWA PAUNI MIL 26 KUMNG'OA AGUERO MAN CITY

KIBIBI kizee cha Turin, Juventus wanajiandaa kutuma ofa ya pauni mil 26 wakitaka saini ya straika wa Manchester City, Sergio Aguero.

Taarifa za ndani ya klabu ya Juve zimesema kuwa Aguero amewekwa katika orodha ya wanandinga wanaowaniwa na vinara hao wa serie A.

Awali, Juventus walimweka katika orodha ya usajili wa majira ya kiangazi mwaka jana, lakini tarifa za sasa zinasema kuwa wanamwania straika huyo katika usajili wa kiangazi.

Lakini hatua ya Juve inaweza kudunda kwa sababu bosi wa matajiri hao wa jiji la Manchester, Pep Guardiola amekana kila hatua ya kuondoka kwa mchezaji yeyote katika kikosi chake.

Akinukuliwa, Guardiola alisema klabu yake haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo nba kwamba bado yuko katika mpango wake wa kusuka kikosi cha ushindani msimu ujao.

“Sitotaka kuona ninamwacha mchezaji muhimu katika kipindi hiki cha usajili wa kiangazi, badala yake ninajipanga kwa ajili ya usajili wa maana.”


“Ninajipanga kwa ajili ya kufanya usajili mkubwa wa majira ya kiangazi na huo ndio msimamo wangu na ninasimama katika ukweli huo,” alisema Pep.

No comments