JUX AMKUMBUSHA DOGO JANJA UMUHIMU WA KUREJEA "SKONGA"

RAPA Jux ambaye amehitimu shahada ya Computer Science katika chuo kikuu cha Guangdong kilichoko Guangzhou, China amekuwa chachu ya msanii mwenzake Dogo Janja kukumbuka kurudi shule.

Dogo Janja licha ya kumpongeza Jux kwa hatua hiyo, hakusita kuelezea kilichoko moyoni mwake kwa kusema anatamani siku moja arudi shule.

“Kwanza napenda kumpongeza Juma Jux kwa kuhitimu masomo yake na ni furaha kuongeza mwanamuziki msomi katika kiwanda cha muziki wa bongofleva,” alisema Dogo Janja.

“Bongofleva ni kitu kikubwa sana, natamani siku moja nirudi shule kwani ndio ndoto niliyonayo ili siku moja niweze kuhitimu kwa ngazi ya shahada,” aliongeza rapa huyo.   


“Kitu ninachoweza kusema ni kwamba muda wowote kuanzia sasa naweza kurudi shule kwa sababu ni kitu ambacho kinaniumiza sana kwenye maisha yangu nikiona wenzangu kama hivi.”

No comments