KAMA BADO HUJAUPATA WIMBO “MBEGU CHUNGU” WA FABRICE KULIALIA, BASI UPAKUE HAPA
Huyu ni mkali wa masauti aliyetamba sana na bendi ya Akudo Impact. Anaitwa Fabrice Kulialia, kwa sasa yupo na Maunt Meru Rickernest Music Band ya Arusha.

Miezi michache iliyopita, Fabrice Kulialia ambaye kwa wakati fulani aliitumikia pia bendi ya Malaika, aliachia nyimbo zake kadhaa ukiwemo huu utakaousikiliza hapa “Mbegu Chungu”.

Kulialia ameiambia Saluti5 kuwa lengo lake ni kutengeneza albam ambapo kwa kuanzia ametanguliza silaha zake tatu za kufanyia promosheni albam yake.

Leo tunaanza na wimbo “Mbegu Chungu” ambapo ndani yake utamsikia Kulialia anavyolia juu ya mapenzi huku akisaidiwa na waimbaji mafundi akiwemo Katoto Maya.

No comments