Habari

KAMATI YA USAJILI NA YA UFUNDI SIMBA ZAPISHANA KUHUSU BOUKUNGU KUBAKI AU KUONDOKA

on

BEKI mkongwe Janvier Besala Boukungu ni
sawa na “home work” kwa Kamati ya Usajili na ile ya ufundi ya Simba.
Kwamba abaki au aende, hakuna
ambae ana uhakika wa asilimia kwa kuwa kuna mambo yanachanganya.
Imeelezwa kati ya wajumbe, wapo
wanaoona wakati umefika aende na wengine wanaona angalau msimu mmoja aongezewe.
“Unajua kweli umri wa Boukungu
umekwenda, lakini alionyesha weledi sana. Uwanjani alijituma na nje ya uwanja
alikuwa ni professional kabisa,” kilieleza chanzo.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili
wa Simba, Zacharia Hans Poppe yeye alisema kazi ya Boukungu ilikuwa bora na
wanaona atabaki lakini kuna viongozi wanaamini ni vyema wakamruhusu kwa heshima
na wakampongeza kwa kazi yake nzuri ili aondoke.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *