KAPOMBE, MANULA WAKAMILISHA YAO "KIMYAKIMYA" MSIMBAZI

NYOTA wawili wa klabu ya Azam FC, Shomari Kapombe na Aishi Manula ni kama mambo yao yameshakamilika katika klabu ya Simba.

Habari zinasema kwamba Kapombe na Manula wamekubaliwa na klabu yao ya Azam kuhamia Simba baada ya wote wawili kubakiza mikataba yao muda usiozidi mwezi mmoja kila mmoja.

“Unajua kuwa hao ni wachezaji halali wa Azam lakini tayari tumekubaliana nao kwamba hawataongeza mkataba katika Azam na wamefikia makubaliano rasmi na Simba,” chanzo kimoja kimesema.


Kapombe ambaye ni beki mwenye uwezo wa kucheza namba zote za nyuma, anasajiliwa rasmi kwa sababu ya kuimarisha ukuta wa Simba wakati kipa Manula anakuja kuimarisha nafasi hiyo ambayo kwa sasa ina makipa watatu; Mghana Daniel Agyei, Peter Manyika na Denis Richard.

No comments