KAPOSHOO: KANUMBA ALIPANGA KUNIFANYIA MAKUBWA KWENYE FILAMU …kifo chake kikakatisha ndoto kubwa


Mpiga tumba wa FM Academia, Paul Nsigayehe “Kaposhoo” amesema marehemu Steven Kanumba alipanga kumfanyia makubwa kwenye filamu lakini bahati mbaya kifo chake kikakatisha mipango yote.

Akiongea na kipindi cha Afro TZ cha Radio One, Jumanne usiku, Kaposhoo akafichua kuwa mbali na muziki, pia ni mwigizaji mzuri wa filamu.

Kaposhoo aliyetamba pia na Twanga Pepeta akasema alishiriki kucheza filamu za vichekesho na kundi la Futuhi cha Mwanza.

Aidha Kaposhoo akadai kuwa alimfuata Kanumba na kumjuza juu ya kipaji chake na kuahidiwa kuingizwa kwenye moja ya filamu za Steven Kanumba.

“Kanumba alipanga kunitoa na tayari alishaniandalia filamu lakini kwa bahati mbaya akafariki muda mfupi kabla hatujaanza kucheza filamu hiyo,” alisema Kaposhoo.

No comments