KASEBA ATAFUTA MAPAMBANO YA KIMATAIFA KUMUANDAA BINGWA WAKE WA AFRIKA

MSIMAMIZI wa mchezo wa kickboxing nchini, Japhet Kaseba amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutafuta mapambano ya kimataifa kwa ajili ya kumwaandaa bingwa wa Afrika wa mchezo huo, Jeremiah Naasari.

Akiongea na saluti5, Kaseba alisema kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kushiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huo hivyo anahitaji mapambano mengi ya kumweka sawa.

Alisema, tayari mchakato wa kuandika barua za maombi ya mapambano hayo umefanyika ikiwa ni pamoja na kuomba mapambano ya mabondia kutoka nchi za Malaysia, Japan, China na nyingine nyingi.


“Hivi sasa nguvu nimeelekeza katika kumwandaa bingwa wetu wa Tanzania na Afrika wa kickboxing ambaye anakabiliwa na mashindano ya kimataifa, sasa tunatafuta mbinu itakayomwezesha kufanya vyema,” alisema Kaseba.

No comments