KATIBU WA BASATA ALIPOMTEMBELEA TONGOLANGA SIKU MOJA KABLA YA KIFO CHAKE


Kama ilivyolezwa hapo awali, mwimbaji aliyefanikiwa kuweka muhuri wake kwenye muziki wa dansi kupitia midundo ya sindimba, Halila Tongolanga amefariki dunia baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Tongalanga aliyetesa na wimbo “Kila Munu Ave na Kwao”,l amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya figo.

Juzi Jumamosi, siku moja kabla ya kifo cha Tongolanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo Mngereza, alienda Muhimbili kumjulia hali mwanamuziki huyo.


Mngereza aliandamana na Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Adrian Nyangamalle. 

Pichani juu ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo Mngereza (katikati) na Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Adrian Nyangamalle (kulia) wakimjulia hali Tongolanga. Picha imepigwa na msanii wa zamani Ibony Moalim.

No comments