KAUZU FC YAIBOMOA SHERATON 2-1 NDONDO CUP

VITA ya majirani wa Temeke ilimalizika jana kwenye uwanja wa Tandika Mabatini kati ya FC Kauzu dhidi ya Sheraton FC kwa Kauzu kuibuka na ushindi wa mabao  2-1.

Kauzu walipata bao la kwanza dakika ya tano mfungaji akiwa ni Hamad Kibopile ambaye goli lake ni moja ya magoli mazuri kwenye michuano hii ya Ndondo Cup 2017.

Dakika 23 Kauzu wakafunga bao lao la pili kupitia Awadh said na kuifanya mechi kwenda mapumziko huku kauzu wakiwa mbele kwa magoli 2-0.

Kipindi cha pili Sheraton walikuja juu na kufanikiwa kufunga goli dakika ya 56 na matokeo yakadumu hadi dakika 90.
Mchezo mwingine ulipigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Faru Jeuri dhidi ya Miami na kumalizika kwa timu hizo bila kufungana.


Baada ya michezo ya leo, Kauzu wanakuwa vinara wa kundi H kwa kufanikiwa kupata pointi tatu wakifuatiwa na Faru Jeuri na Miami ambao wote kwa pamoja wana pointi moja moja huku Sheraton wakiwa mkiani mwa kundi hilo.

No comments