KIPA THIBAUT COURTOIS AITINGISHIA KIBERITI CHELSEA... akausha kufafanua msimamo wake kuhusu kubaki

MLINDA mlango Thibaut Courtois ni kama ameamua kutingisha kiberiti ambapo sasa hajaweka bayana kama ataendelea kubaki katika kikosi cha machampioni wa premier, Chelsea.

Taarifa za hadi mwishoni mwa wiki zinasema kuwa Thibaut Courtois alikwamisha mazungumzo ya kurefusha kandarasi yake, ingawa kulikuwa na taarifa kuwa ushawishi kati yake na uongozi unaendelea.

Kisa kilichoelezwa kuwa ni chanzo cha kukwama kwa mazungumzo hayo ni kutokana na mlinda mlango huyo kugomea nyongeza ndogo ambapo wakala wake anaendelea na mazungumzo ya kina kumbadilisha mawazo.

Taarifa za ndani zinasema kuwa huenda hatua ya Courtois kugoma kuongeza kandarasi inatokana na ukweli kuwa yumo katika mpango wa kutaka kuhamia katika kikosi cha mabingwa wa barani Ulaya, Real Madrid.

Klabu ya Real Madrid imeweka bayana azma ya kutaka kumng’oa mlinda mlango huyo, hivyo wameongeza ushawishi wa kutaka saini yake klatikia kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa mgomo huo, kocha Antonio Conte yumo katika mazungumzo na mlinda mlango wa AC Milan, Gianluigi Donnaluma kama njia ya kutaka kuziba pengo la Thibaut Courtois endapo ataendelea kuidengulia Chelsea.


Kuna taarifa kuwa Donnaluma nae amekataa kusaini kandarasi mpya ndani ya AC Milan, hivyo ni dalili kuwa huenda akakamilisha dili la kutua Chelsea.

No comments