KIPA WA KAGERA SUGAR AKIRI KUMUOGOPA AMISI TAMBWE

KIPA wa timu ya Kagera Sugar, Hussein Sharif “Casillas” amesema kuwa alikuwa akimuhofia mshambuliaji wa klabu ya yanga, Amisi Tambwe raia wa Burundi kila alipokutana nae uwanjani wakati wa mechi.

Kipa huyo ambaye msimu huu haukumwendea vyema baada ya kusimamishwa na uongozi wa klabu ya Kagera Sugar kwa madai ya kuihujumu timu, amesema kuwa alikuwa akimuhofia Tambwe asimfunge.

“Tambwe ni mshambuliaji hatari, ni mjanja na mwenye maarifa makubwa anapolikaribia goli, kwa kweli nilikuwa nikimuhofia sana,” alisema kipa huyo.

“Tangu nilipokuwa Mtibwa Sugar sikutaka kabisa kufungwa na Tambwe lakini ilishindikana kumzuia asifanye anachokitaka,” aliongeza.


Casillas kabla ya kutua kwenye kikosi cha timu ya Kagera, aliwahi kuitumikia klabu ya simba ambayo ilimnasa kutoka Mtibwa Sukari ya Morogoro.

No comments