KLOPP ATILIA MKAZO HARAKATI ZAKE ZA KUSAJILI MLINDA MLANGO

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kuwa mpango wake wa kusajili mlinda mlango ni wazo endelevu na watatimizi azma hiyo muda ukifika.

Hii ni kutokana na kile alichoeleza kuwa kikosi chake kinatakiwa kuwa kipana kwa ajili ya Ligi ya premier msimu ujao.

Lakini pia sio kwa ajili ya Ligi pekee bali kocha huyo ameweka bayana nia yake ya kutaka kushiriki kwa ushindani mkubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwakani.

Liverpool msimu huu imefanikiwa kuwemo katika orodha ya timu zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi ya premier.

“Nitakamilisha usajili wa mlinda mlango wa maana katika usajili huu au ujao, kwasababu tunahitaji kusuka kikosi bora cha ushindani ndani na nje ya Ligi ya premier msimu ujao.”

“Nafikiri tunahitaji mlinda mlango kwa kasi, kikubwa inategemea na aina ya mahitaji tuliyonayo kwa sasa,” alisema Klopp.

“Kwa vyovyote bado tuko chini, tuna walinda mlango nyuma, tunahitaji kuangalia maendeleo ya klabu.”


“Lakini kwa vyovyote vile hatuna sababu ya kusubiri kuangalia kupata mlinda mlango wa kuleta changamoto ya kuimarisha kikosi,” alisisitiza kocha huyo wa majogoo wa jiji la London.

No comments