KLOPP AWEKA MEZANI PAUNI MIL 22 AKIWANIA KUBOMOA UKUTA WA PORTO

MAJOGOO wa jiji la London wameweka mezani dau la pauni mil 22 kwa ajili ya kusaka saini ya mlinzi wa kati wa timu ya Porto ya Ureno, Felipe Monteiro.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amenukuliwa hivi karibuni akiweka wazi kuwa, anahitaji saini ya mlinzi huyo.
Klopp amebaini mapungufu makubwa katika safu yake ya ulinzi, hivyo anaamua kuingia sokoni kwa ajili ya kusuka kikosi na sasa anaanza kumfukuzia Monteiro.

Beki huyo kisiki raia wa Brazil amekuwa katika kiwango cha hali ya juu kiasi cha kuzivutia klabu mbalimbali za Ulaya.

Tayari kuna tetesi za klabu nyingine kumwania, zikiwemo Tottenham, Westham pamoja na Manchester United.


Awali Liverpool waliweka mezani dau la mil 15 kwa ajili ya mlinzi huyo, lakini Porto hawakusikika wakitamka lolote licha ya kunukuliwa mara kadhaa.

No comments