KOCHA GEORGE LWANDAMINA AMTAKA MBARAKA YUSUPH YANGA

KAMATI ya Usajili Yanga imekutana na kuchambua majina ya wachezaji ambao inawahitaji huku ikipendekezwa kutoa kipaumbele kwa wachezaji vijana zaidi.

Kamati hiyo ilikutana hivi karibuni na kupitisha majina ya nyota inaowahitaji baada ya kupitia ripoti toka kwa kocha wa mabingwa hao, George Lwandamina.

Miongoni mwa vijana ambao Yanga inatarajia kuwasajili ni pamoja na nyota wa timu ya Kagera Sugar na timu ya Taifa, Mbaraka Yusuph.

Nyota huyo ambaye ameshateta na vigogo wa Kamati ya Usajili yanga na kukamilisha hatua zote, kwa hivi sasa yupo nchini Misri na timu ya taifa.


Yanga imepania kukifumua kikosi chake upya baada ya wachezaji wengi, hasa wa kulipwa, kumaliza mikataba yao. 

No comments