KOCHA KALLY ONGALA AMTAMANI AMISI TAMBWE KIKOSINI MAJIMAJI

KOCHA wa timu ya Mjimaji ya Songea, Kally Ongala amesema kuwa anatamani siku moja angefanya kazi na mchezaji wa Yanga, Amisi Tambwe raia wa Burundi.

Ongala ambaye amewahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma alisema, kama angekuwa na Tambwe kwenye kikosi chake msimu uliopita wangefanya vizuri zaidi.

“Tambwe ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, binafsi natamani kufanya nae kazi katika kikosi changu endapo timu yake itaamua kuachana nae,” amesema Ongala.

Kocha huyo aliyefanikiwa kuinusuru Majimaji isishuke daraja msimu uliopita, alisema kuwa timu yake inakosa mshambuliaji mwenye uzoefu kama wa Tmbwe, hivyo kumpata yeye inaweza kuwa msaada tosha.


Amisi Tambwe amekuwa akipata wastani mzuri wa mabao kila msimu ambapo kwa msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 11 na kukamata nafasi ya tatu.

No comments