KOCHA WA COLOMBIA AWAMBIWA JAMES RODRIGUEZ: TUMIA AKILI, ‘TIMKA’ REAL MADRIDKOCHA wa timu ya taifa ya Colombia, Jose Peckerman amemshauri straika James Rodriguez kuachana na Real Madrid kiangazi hiki na kujiunga na klabu nyingine ili kufufua kipaji chake. 

Peckerman anasema: “Ni ajabu kwamba mchezaji wa kiwango hicho hawezi kucheza mara nyingi zaidi… Kwa ajili ya timu ya taifa ya Colombia, ni vizuri kwa James kucheza mara kwa maraSitaki kuchukua jukumu la kumwambia mambo ya kufanya, lakini anajua nini kinahitajika ili kutatua hali yake.”

Straika huyo wa miaka 25 aliyeanza mara 25 tu katika mashindano yote msimu uliopita, anaonekana si hitaji muhimu Bernabeu na alienguliwa katika kikosi cha Zinedine Zidane kilichocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mapema mwezi huu.

Rodriguez amekuwa akiporomoka taratibu tangu aliposajiliwa kwa pauni milioni 70 kutoka Monaco baada ya kufanya mambo makubwa katika Kombe la Dunia 2014, lakini klabu kibao kubwa Ulaya zikiwamo Manchester United na Chelsea zinafuatilia mwenendo wake Real na Peckerman anaamini staa wake huyo anahitaji kuondoka ili kuokoa kipaji chake.

No comments