KRC GENK YAMKOSESHA MBWANA SAMATTA KAMBI YA TAIFA STARS MISRI

KIKOSI cha timu ya taifa “Taifa Stars” kimeondoka Jumanne kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho huku ikiwa bila ya nahodha wake, Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji.

Taifa Stars inatarajia kushuka dimbani Juni 10 kumenyana na Lesotho katika mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini dare s Salaam.

Samatta ameshindwa kujumuika na wenzake baada ya kutingwa na majukumu ya klabu yake ya KRC Genk ambayo inasaka tiketi ya kwenda kwenye michuano ya Kombe la Europa msimu ujao.

Mbali na Samatta, Mtanzania mwingine anayecheza soka la kulipwa nchini Sweden, Farid Mussa amethibitisha kuwa ataungana na wenzake nchini Misri kwa ajili ya kambi ya muda mfupi.

Timu ya taifa iliondoka Jumanne kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya siku saba kabla ya kucheza na Lesotho.  

No comments