KUJIUZULU UENYEKITI KWA MANJI KWALIPUA FURAHA MSIMBAZI

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kuwa wamepata amani baada ya kusikia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji ametangaza kujiuzulu.

Hans Poppe amesema kuwa Manji amekuwa akiwatesa kwa muda mrefu tangu aingie kwenye uongozi ndani ya klabu ya Yanga na hasa wakati wa usajili wa wachezaji muhimu.

“Taarifa za kuondoka kwa Manji tumezipokea vizuri sana kwa sababu ndio mtu aliyekuwa anatusumbua katika usajili tangu siku ya kwanza alipoingia madarakani,” alisema Hans Poppe.

“Ilikuwa vigumu kupambana na uwezo wa kifedha wa Manji na hasa linapokuja suala la kugombea wachezaji muhimu kwa timu.” “Manji aliwahi kumliza aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage wakati wa kumsajili beki kisiki, Mbuyu Twite kutoka kwenye klabu ya APR ya Rwanda.”

“Akiwa ana imani kuwa Twite atajiunga na Sim,ba mambo yaligeuzwa ghafla na beki huyo kutua mikononi mwa Yanga.”
“Ni tukio ambalo lilimliza Rage kipindi hicho akiwa mwenyekiti wa Simba na kuwakera mashabiki wao.”

Yanga pia iliwahi kuwazidi kete tena Simba kwa kumchomoa beki wao tegemeo, Kelvin Yondan kutoka kwenye kambi ya timu ya Taifa Stars na kujiunga na Yanga juu kwa juu.    

Kitendo hiki kiliwakera viongozi wa Simba ambao walilalamika kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF), lakini hawakufanikiwa kwani Yondani anaendelea hadi leo kukipiga Yanga.   

Uongozi wa Simba sasa unaonekana kuchekelea baada ya Manji kutokuwepo kwenye harakati za usajili.

No comments