LEICESTER YAINGIA VITANI KUMWANIA KIUNGO ALVARO GONZALEZ WA VILLAREAL

LEICESTER City wanapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia kiungo wa Villareal, Alvaro Gonzalez.

Lakini wanalazimika kuweka dau la ziada mezani la pauni mil 24 kwa ajili ya jembe hilo.

Alvaro Gonzalez amekuwa akihusishwa na kujiunga na Leicester City katika usajili ujao wa dirisha la majira ya joto.

Awali Spur pia waliweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya Gonzalez kabla Atletico hawajaweka bayana kuwa dau la kiungo huyo ni mil 23.

Leicester wanakomaa na dau la awali lakini wakaweka bayana kuwa wanaweza wakaongeza kiasi cha pauni mil 2 ili dili kufikia pauni mil 12.


Alvaro Gonzalez amekuwa katika kiwango bora katika kipindi cha miaka miwili hii na kuwa na uhakika wa kuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

No comments