LORIS KARIUS AJIPA UHAKIKA WA KUENDELEA KUWA KIPA NAMBA MOJA LIVERPOOL

KIPA wa Liverpool Loris Karius amesema kwamba ingawa katika kikosi chake kuna changamoto nyingi, lakini anajua ataendelea kudaka.

Akiongea juzi kipa huyo wa zamani wa klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani ya Mainz amesema kwamba pamoja na changamoto nyingi ambazo zinamkabili lakini anataka kubaki kuwa kipa namba moja katika kikosi hicho cha klabu ya Merseyside.

Wakala wa mchezaji huyo, Florian Goll amesema habari kwamba mchezaji wake anataka kurudi Ujerumani ni za uongo.

Wakala huyo amesema kwamba anajua kuwa mchezaji huyo ana changamoto kubwa kutoka kwa kipa mwingine, Simon Mignolet lakini mawazo yake ni kwamba atabaki Liverpool.

Amesema kwamba Karius ni kipa mzuri lakini pamoja na mwenzake Simon Mignolet wanatakiwa kupambana kwa ajili ya Liverpool.

Karius ambaye amepoteza kuwa kipa namba moja wa kikosi hicho, amekuwa akitajwa kwamba anataka kurudi Ujerumani, lakini wakala wake amesema kwamba kipa huyo atabaki Liverpool.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa hajawahi kukosa imani na kipa huyo na kwamba ikiwa yeye mwenyewe anataka kurejea Ujerumani, hiyo ni habari nyingine.


“Sina hakika kama anataka kuachana na Liverpool, lakini kwa upande wangu sijawahi kukosa imani nae. Ndio, kuna wakati kipa lazima apoteze namba kwa mpinzani wake, lakini haina maana kwamba kipa huyo sio bora,” amesema Klopp.

No comments