LUIS FIGO ASEMA RONALDO HATA AKISEPA REAL MADRID "POA TU"

LICHA ya kuwepo na tetesi zinazomuhusisha nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuwa anaweza kuitema klabu hiyo na hivyo kuwa pigo kubwa kwao, lakini staa wa zamani Luis Figo ameibuka akisema kuwa hakuna mtu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika na hivyo akiondoka poa tu.

Hadi sasa bado Ronaldo hajaweka wazi kuhusu hatma yake baada ya wiki iliyopita kudaiwa kuwa anaweza kuitema klabu hiyo ya Santiago Bernabeu.

Kutokana na kile ambacho inadaiwa kuwa haimlindi katika sakata lake la ukwepaji kodi ya kiasi cha pauni mil 13.

Kutokana na sekeseke hilo, klabu yake ya zamani ya Manchester United na Paris Saint Germain ndizo zinazotajwa kuwa huenda staa huyo mwenye umri wa miaka 32 akakimbilia huko.

Pamoja na taarifa hizo, mapema wiki hii rais wa Real Madrid, Florentino Perez alisema kuwa hawana mpango wa kuiuza hazina yao hiyo kuu lakini Figo anaonekana kupingana nae baada ya kusema hakuna mchezaji ama mkurugenzi ambaye anaweza kuwa mkubwa wakati anapojiunga na mabingwa hao wa La Liga na Ulaya.

“Haya ni maoni yangu kwamba hakuna mchezaji ambaye nafasi yake haizibiki na hata kama akiwa ni Cristiano Ronaldo,” Figo aliuambia mtandao wa Goal wakati alipoulizwa kuhusu hatma ya straika huyo wa Ureno.

“Klabu haiwezi kumtegemea mtu mmoja, historia ya klabu kama hii iko juu ya kila mmoja, hata awe mkurugenzi ama mtu gani,” aliongeza staa huyo wa zamani.


Mbali na hilo alisema kuwa licha ya wengine kudai kuwa Real Madrid haitaweza kufanya vyema bila ya Ronaldo lakini Figo anasema kuwa hilo halimuingii kichwani kama mshindi huyo wa tuzo ya 2016 Ballon d’Or ambaye anapewa nafasi ya kuinyakuwa tena mwaka huu anaweza kuondoka.

No comments