LWANAMINA AWEKA KILA KITU MIKONONI MWA VIONGOZI WA YANGA

KABLA ya kuondoka kuelekea nchini Zambia, kocha wa timu ya Yanga, George Lwandamina alikabidhi ripoti yenye orodha ya mapendekezo ya wachezaji anaowahitaji.

Kamati ya usajili wa Yanga imeanza kufanyia kazi mapendekezo ya Lwandamina kwa kusaka nyota wapya ndani na nje ya nchi.

Katika ripoti ya kocha huyo, aliyataja baadhi ya maeneo kuwa ni nafasi ya kiungo mkabaji, beki wa pembeni, kipa na mshambuliaji mmoja.

Baadhi ya nyota wa Yanga wamemaliza mikataba yao lakini wapo ambao wataongezewa muda wa kuichezea klabu hiyo kulingana na mahitaji ya kocha lakini pia wapo watakaoachwa.


Baada ya kuvunjwa kwa kambi ya timu ya taifa, kila kitu kinatarajiwa kuwekwa wazi na kamati ya usajili kwani wachezaji wengi muhimu wamekwenda kwenye majukumu ya timu zao za taifa.

No comments