MAJERUHI JAMAL MNYATE AHOFIA KUTEMWA KIKOSINI SIMBA SC

WINGA wa Simba, Jamal Mnyate amehofia kutemwa katika kikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kuwa majeruhi wa goti kwa muda mrefu.

Akiongea jana na saluti5, Mnyate alisema kuwa kitendo cha kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kina athari kubwa kwa mchezaji hasa anayechezea timu kubwa kama Simba.

“Sijajua kama nitakuwepo hapa kwa msimu ujao, nasubiri jibu la kocha kama atakubali kuendelea na mimi katika mipango yake,” alisema Mnyate.

Alisema, mchezaji anapaswa kuwa fiti wakati wote kama mwanajeshi anayesubiri amri kutoka kwa kamanda wake kupambana na vita.


Mnyate alisema alianza vyema mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, lakini alipata majeruhi ya goti mzunguuko wa pili na kupoteza namba katika kikosi cha kwanza.

No comments