MAJIMAJI YATHIBITISHA KUENDELEA KUMUHITAJI KALLY ONGALA MSIMU UJAO

BAADA ya kuinusuru kushuka daraja kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao umefikia tamati kwa Yanga kubeba ubingwa, klabu ya Majimaji imeweka wazi nia ya kutaka kuendelea kufanya kazi na kocha wake, Kally Ongala.

Kally ambaye amewahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma, alichukuliwa na majimaji kwa ajili ya mipango ya muda mfupi huku wakiwa na lengo la kutaka awabakize kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara.

“Tumefanya nae kazi kwa mafanikio, ni kocha ambaye tunahitaji aendelee kubaki hapa kwa msimu mwingine zaidi,” alisema mwenyekiti wa klabu hiyo, Humphrey Milanzi.

“Unaweza kuona namna alivyopambana kwenye mazingira magumu kuhakikisha timu inafanya vizuri katika hatua za lala salama, ni kocha ambaye hatuna mpango wa kuachana nae.”


Kally Ongala amefanikiwa kuiongoza Majimaji isishuke daraja msimu huu na kuziacha timu za African Lyon, Toto Africa na JKT Ruvu zikienda na maji.

No comments