MALIMI BUSUNGU MBIONI KUTIMKIA AFRIKA KUSINI

MSHAMBULIAJI aliyemaliza muda wake wa kuitumikia klabu ya Yanga, Malimi Busungu yuko kwenye mipango ya kutimkia Afrika Kusini kusaka ulaji mpya.

Mshambuliaji huyo amefikia uamuzi huo baada ya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga huku kukiwa na hali ya sintofahamu kati yake na kocha msaidizi, Juma Mwambusi.

Chanzo cha taarifa hiyi kinaeleza kuwa nyota huyo aliyewika na timu ya Mgambo ya Tanga kabla ya kutua Yanga yuko katika hatua za mwisho za kutimkia Afrika Kusini.

“Amemaliza mkataba Yanga na hivi sasa jicho lake linatazama kwenda nje ya nchi kusaka malisho mapya,” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.


Busungu tangu apate ajali ya gari Mikumi Morogoro amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

No comments