MAN UNITED WASITEGEMEE SANA KATIKA KUMSAJILI GRIEZMANN, HUENDA ASICHOMOKE TENA ATLETICO

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amedokeza kwamba huenda asiihame klabu yake licha ya kwamba anatafutwa na klabu nyingine kubwa Ulaya, ikiwemo Manchester United.

Mfaransa huyo mwenye miaka 26, aliandika kwenye Twitter “Sasa zaidi ya zamani! Mimi na Real Madrid tuko pamoja.”

“Hapa ni nyumbani na nimezoea kuwa hapa, hivyo hii ni familia yangu na nitaendelea kuwa nayo kwa muda mrefu katika maisha yangu,” aliandika.

Aliandika hayo saa chache baada ya marufuku ya klabu hiyo kuzuia kununua wachezaji kudumishwa.

Hii ina maana kwamba huenda klabu hiyo isiweze kumnunua mchezaji mwingine iwapo itamuuza.

Alhamisi ilibainika kwamba Manchester United nao pia wanaonekana kupunguza hamu ya kutaka kumnunua.

Kwa kuwa Atletico haiwezi kununua wachezaji wengine hadi Januari, inatarajiwa kwamba Griezmann atapewa mkataba mpya.

United walitaka sana kumnunua mshambuliaji huyo na walikuwa wanatafakari uwezekano wa kufikisha euro mil 100 kumfungua kutoka kwenye mkataba wake.

Lakini duru zinasema ununuzi wa Griezmann sasa si kipaumbele kwa united.

Inafahamika kwamba kuumia kwa Zlatan Ibrahimovic kumeifanya klabu hiyo ya Manchester United kutafakari upya msimamo wake,huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mkataba wa raia huyo wa Sweden unaomalizika Juni 30.

Hata akipewa mkataba mpya, hataweza kucheza hadi Januari. 

United sasa wanadaiwa kumtafuta mshambuliaji mkuu badala ya mchezaji wa kawaida namba 10 na wanaamini tayari wana wachezaji wa kutosha kujaza nafasi hiyo.


United wasipompata Griezmann kuna baadhi ya wanaosema huenda wakamtafuta Romelu Lukaku wa Everton au Andrea Beloti wa Torino, wanaweza pia kumtafuta Alvaro Morata wa Real Madrid.

No comments