MANCHESTER CITY WAMTENGEA OUSMANE DEMBELE MKWANJA WA PAUNI MIL 35

MANCHESTER City wanatambua kuwa Ousmane Dembele ni kati ya wachezaji wa kiwango bora katika ufumaniaji nyavu, hivyo wameamua kuweka mkwanja mezani ambapo wametenga kitita cha mil 35.

Kinachoendelea kwa sasa kwa matajiri hao wa jiji la Manchester ni kujipanga kwa ajili ya kupiga hodi katika klabu ya Borrusia Dortmund huku wakijua kuwa kandarasi ya straika huyo bado ipohadi mwaka 2021.

Pamoja na kutambua hilo, mawakala wa City wameamua kwenda kuketi na kuibuka na azimio la kukomaa nae japo wanakiri ugumu wa kukamilika kwa dili hilo.

The Sky imenukuu tovuti ya klabu ya Manchester City iliyosema kuwa uongozi wa juu wa matajiri hao wameidhinisha dau la kuweka mezani ambalo ni nono.

Taarifa ya klabu hiyo imethibitisha kuweko kwa mazungumzo ya awali baina yao na rais wa Dortmund, Reinhard Rauball.

Kikao cha kuhusiana na mazungumzo hayo kiliketi Jumatatu nchini Ujerumani na sasa ni juu ya klabu ya Dortmund kufungua mazungumzo ya mwisho.

Nyota huyo tayari ameonyesha dalili za kukubali dili la kuhamia Manchester City na hata dau lake meliweka bayana pia.

Dau hilo linakuja katika muda ambao klabu ya Cityinatarajia kuketi tena na Wajerumani hao kabla ya kuanza kwa wiki inayoanza Jumatatu ijayo.

Ingawa taarifa za ndani ya timu hiyo ya Bundesliga inaonyesha ugumu wa kumwachia straika huyo, lakini City wanatumia kishawishi cha mkwanja kwa ajili ya kuilazimisha Dortmund.

City imeonyesha utayari wa kuweka mezani kiasi kisichopungua pauni mil 35 kwa mfumania nyavu huyo, huku kiwango cha kila wiki kikiwa ni pauni 170,000.


Pamoja na City, pia mabingwa wa Ulaya Real Madrid nao wameingia katika mbio za kuwania saini ya Dembele.

No comments