MANCHESTER UNITED SASA ISHINDWE YENYEWE KWA ERIC DIER WA TOTTENHAM


MANCHESTER UNITED imeripotiwa kuambiwa na Tottenham kwamba inaweza kupata huduma ya kiungo wake wa ulinzi, Eric Dier kiangazi hiki kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 50.

Dier, 23, anayemudu pia beki ya kati, anaelezwa kuwa miongoni mwa malengo kipaumbele kwa Jose Mourinho, ambaye tayari ameweka wazi kwa waajiri wake kwamba anamtaka nyota huyo wa kimataifa wa England kwa ajili ya kuchukua nafasi ya veteran Michael Carrick aliyeongezewa mwaka mmoja katika mkataba wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph, Tottenham inaamini haina ubavu wa kuzuia kumpoteza mchezaji wake muhimu kwa timu pinzani katika mbio za ubingwa, na United inaelezwa kutaka kupunguziwa bei imalize biashara baada ya kukataliwa dili la thamani kama hiyo katika usajili wa Januari.

Kwa sasa Dier anavuna mshahara wa pauni70,000 kwa wiki akiwa na Spurs na kuna uwezekano mkubwa akalipwa mara mbili zaidi kama atatua Old Trafford.

Hata hivyo Daily Mail lenyewe limeandika kuwa Tottenham haina mpango wa kutaja bei ya kiungo huyo kwa kuwa haifikirii kumweka sokoni.

No comments