MANCHESTER UNITED YAPATA KIWEWE CHA CRISTIANO RONALDO


Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekereka sana baada ya kutuhumiwa kwamba alifanya ulaghai wakati wa ulipaji ushuru na anataka na sasa kuihama klabu hiyo.

Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghai wa kutolipa mamilioni ya ushuru. Hata hivyo Ronaldo amepinga tuhuma hizo.

Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo ya Madrid una kifungu cha euro bilioni moja (£874.88m), ambacho kinafaa kufikishwa ndipo afunguliwe kutoka kwa mkataba wake.
Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa kwa pauni milioni 80, alitia saini mkataba wa miaka mitano katika klabu hiyo Novemba mwaka 2016.
Mreno huyo sasa anahusishwa na uhamisho wa kurejea Manchester United ambayo italazimika kulipa pauni milioni 70 hadi 80 ili kumnasa mkali huyo.
Aidha, United italazimika kumlipa Ronaldo mshahara usiopungua pauni 365,000 kwa wiki.
Ronaldo, aliyewasaidia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhumiwa kulaghai maafisa wa serikali ushuru wa takriban euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya 2011 na 2014.
Msimu wa 2016-17, Ronaldo alisaidia Real kushinda taji la ligi Uhispania wka mara ya kwanza tangu 2012, na pia kutetea taji lao la Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.
Ronaldo, aliyeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya pia akiwa na Manchester United mwaka 2008, amefunga mabao 105 katika michuano hiyo, 11 zaidi ya mpinzani wake wa Barcelona Lionel Messi.
Tayari mashabiki na wachambuzi wanazi wa Manchester United wameanza kuingiwa na kiwewe cha kumuona Ronaldo akirejea Old Trafford.
Baadhi ya wachambuzi wameorodhesha sababu kibao za kwanini Manchester United wanastahili kumsajili tena Ronaldo.

No comments