MARYAM CHARLES ASEMA NOLLYWOOD YABISHA HODI HOLLYWOOD

STAA wa filamu, Maryam Charles amesema kuwa filamu za Nigeria zimepiga hatua kubwa sana na kuna uwezekano zikaingia kwenye soko la Marekani.

Staa huyo alisema kuwa ubunifu kwenye tasnia ya filamu inatia moyo kuanzia kwenye ngazi ya uigizaji hadi Studio zinazotumika.

“Ni kweli Hollywood wako mbali sana kwa sababu ya vifaa wanavyotumia na uwekezaji mkubwa wa fedha, lakini hata Nollywood naona inaelekea huko.”

“Ni vigumu kupata soko kwenye taifa kubwa kama Marekani lakini kuna dalili ya kufia huko kwa sababu ya ubora wa kazi zetu,” alisema staa huyo.


Filamu za Nigeria zimejipatia soko kubwa barani Afrika baada ya kuanza lakini zinalaumiwa kwa kuwa na maudhui yanayofanana.

No comments