MASHABIKI WA AZAM FC WAMUOMBA RADHI JOHN BOCCO KWA KUACHWA KATIKA MAZINGIRA "MABAYA"

BAADA ya timu ya Azam kuachana na mshambuliaji wake mkongwe zaidi, John Bocco “Adebayor”, mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa maoni tofauti kutokana na uamuzi huo.

John Bocco ndie mchezaji aliyedumu zaidi kwenye kikosi hicho baada ya kupanda nae daraja lakini mwishoni mwa msimu huu aliachwa katika mazingira ya kutatanisha.

“Ni kawaida kwa wachezaji kuondoka timu moja kwenda nyingine, lakini namna alivyoondoka Bocco inasikitisha sana,” alisema shabiki wa klabu hiyo anayejulikana kwa jina la Issa Azam.

“Ametoka mbali na timu hiyo, alistahili kuagwa kwa heshima na kupewa mechi ya kumuaga uanjani, lakini hakuna namna imeshatokea.”


“Tunajua umuhimu wa Bocco na tunajua anatusaidiaje na alipoitoa timu. Ni mchezaji mwenye nidhamu Tanzania nzima, ana historia ya kuzifunga Simba na Yanga kila siku lakini mwisho wa siku historia yake imeishia pale, tunamuomba nay eye atusamehe.”

No comments