MAXIME AAMUA KUZOA MABEKI WA ZAMANI WA SIMBA NDANI YA KAGERA SUGAR

TIMU ya Kagera Sugar ya Misenyi, Bukoba mkoani Kagera imeendelea kukiboresha kikosi chake baada ya kufanikisha usajili wa mabeki nguli wa zamani wa Simba SC.

Kikosi hicho kimemalizana na mlinzi mkongwe, Juma Said Nyoso ambaye alifungiwa kucheza soka ndani na nje ya nchi.
Nyoso alifungiwa na Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF), kwa kosa la kumtomasa makalioni nahodha wa Azam FC, John Bocco “Adebayor”.

Nyoso baada ya kuachwa na Simba alijiunga na Coastal Union ya Tanga akiwa sambamba na swahiba wake, Haruna Moshi “Boban”.

Mbali na Nyoso, Kagera Sugar imeamua kumnasa beki mwingine wa zamani wa Simba, Hassan Isihaka aliyekuwa akichezea African Lyon ambayo imeshuka daraja na sasa anaungana na Peter Mwalyanzi ambaye nae alitokea Simba na wote hao wamejiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Meck Maxime ambaye ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka.


Wachezaji wengine waliotua Kagera Sugar ni pamoja na kipa Hussein Kibawa, Omary Digaga, Jafari Kibayi, huku ikisemekana nyota wengine nyota wengine wanatarajiwa kutua kwenye kikosi hicho kilichomaliza kwenye nafasi ya tatu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara wakiwa nyuma ya miamba Yanga na Simba.

No comments