MBAPPE MAJI MAREFU ARSENAL... PSG nayo yatia mguu

GAZETI la Metro limeandika kwamba wakati Paris Saint Germain wakitaka kuvunja kibubu na kumchukua mshambuliaji hatari wa Monaco,  Kylian Mbappe, Arsenal wanajiandaa kutoa dau jipya kumsajili mchezaji huyo, huku kocha Arsene Wenger akiwa na uhakika wa kumpata.

“Mbappe hana tatizo la wazo la kwenda Arsenal, lakini shida iliyoko ni kwamba Arsenal hawana uwezo wa kutoa fedha ambazo klabu nyingine zinamtaka,” limeandika gazeti linguine la Telegraph.

Majuzi Liverpool walitangaza dau la pauni mil 100 kumtaka Kylian Mbappe lakini Monaco walikataa wakisema kwamba pesa yao haitoshi kumuondoa mshambuliaji huyo katika kikosi chao.

Klabu ya Paris saint Germain inaweza kuandika historia ya uhamisho wa wachezaji kwa sasa ikiwa itafanikiwa kumnasa Klylian Mbappe.


Taarifa ya tovuti hiyo iliyotolewa jana imesema kwamba matajiri hao wako tayari kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni mil 119 kumsajili Mbappe mwenye umri wa miaka 18.

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, matajiri hao wa PSG wanataka kuhakikisha kwamba Mbappe anabaki katika ardhi ya Ufaransa, huku wakijua kwamba nyota huyo anawaniwa na miamba mbalimbali wa soka.

No comments