MBARAKA YUSUPH APELEKWA YANGA NA MAMA YAKE MZAZI... apigwa stop kujiunga na Singida United

YANGA imemfuata na kufanya nae mazungumzo ya kina mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph anayekaribia kusaini mkataba wa miaka miwili, lakini mama yake mzazi akasafisha njia akimkataza kinda huyo kuthubutu kuhamia Singida United inayomnyatia.

Akiongea na saluti5, Mbaraka amesema tayari ameshaanza mazungumzo na Yanga na yamefikia katika nafasi nzito ambapo endapo atakamilisha uhamisho huo anakuja Yanga kufanya kazi ya maana.

Mbaraka amesema amekutana na uongozi wa Yanga, kikubwa umemhakikishia kwamba anahitajika katika kikosi hicho kufuatia kuonwa na kocha wa timu hiyo, George Lwandamina na kwamba ofa hiyo imefuta uwezekano way eye kuhamia Singida United inayonolewa na Has Pluijim.

Kinda huyo amesema hataweza kujiunga na Singida kwa sasa kutokana na zuio alilopewa na mama yake mzazi ambaye amemwambia ni bora akajiunge na Yanga kutokana na Singida kuwa bado ni timu changa ambayo haijaonyesha ukomavu.

“Naweza kwenda Yanga endapo tutamalizana. Nimemalizana nao wanaonyesha nia ya kweli katika kunisajili, naijua Yanga ni timu bora lakini bado kuna Singida pia walinihitaji lakini mama amenizuia nisiende huko,” alisema Mbaraka.


Mama yangu ameniambia kwamba ni afadhali niende Yanga ambayo inajulikana ubora wake na mapungufu yake lakini sio Singida ambayo bado ni timu ndogo inayotakiwa kuangaliwa kwanza ili kujua juu ya uimara wake.”

No comments