MBARAKA YUSUPH: NIKO TAYARI KURUDI SIMBA ENDAPO "TUTAKAMILISHIANA" KABLA SIJADONDOKA SAINI

  
MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa, Mbaraka Yusuph amesema yupo tayari kurudi Simba endapo klabu hiyo itatimiza mahitaji yake kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia.

“Nipo tayari kurudi Simba endapo watakidhi mahitaji yangu,” amesema Mbaraka wakati akizungumza na kutuo kimoja cha radio jana.

Mbaraka alitolewa kwa mkopo kwenda Kagera Sugar lakini baada ya mkataba wake na Simba kumalizika akajiunga moja kwa moja na timu hiyo ambayo imammiliki kama mchezaji wao huku Simba wakisema kwamba bado ni mchezaji wao halali.

“Mimi ni mchezaji halali wa Kagera Sugar, mkataba wangu na Simba ulishamalizika kwahiyo kama wananihitaji inabidi tukae chini na kuzungumza.”

Mbaraka amesema malengo yake katika msimu uliopita yalikuwa ni mfungaji bora lakini hakufanikiwa na badala yake akaishia kufunga magoli 12, magoli mawili nyuma ya Simon Msuva na Abdulrahman Mussa walioshinda tuzo hiyo kwa kufunga magoli 12 kwa msimu mzima.

“Nilipanga niwe mfungaji bora msimu huu lakini kwa bahati mbaya malengo yangu hayajatimia, nashukuru kwa hii tuzo niliyoshinda ya mchezaji bora chipikizi.”

Amekanusha kwamba amesaini na timu ya Yanga na timu nyingine zinazotajwa na kusema kwamba kwavile yeye ni mchezaji huru anaangalia ni mahali gani atakwenda kucheza mpira kwa mafanikio.

No comments