MBIO ZA UCHAGUZI MKUU TFF ZAANZA KUUNDA MAKUNDI KWA WANAOJIPANGA KUWANIA

IKIWA imebakia mwezi mmoja na nusu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa TFF, Agosti 12, tayari makundi yameanza kujipanga ili kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Habari za kuaminika kutoka chanzo cha taarifa hii zina sema kuwa kuna uwepo wa viongozi kadhaa wa soka ambao wamewahi kuitumikia TFF miaka ya nyuma waliojipanga kurudi tena kuwania nafasi mbalimbali za juu ikiwemi ya urais inayoshikiliwa na Jamal Malinzi.

“Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na upinzani mkali kwasababu kuna vigogo waliokuwa TFF zamani wamejipanga kurudi tena na tayari wameanza kuendesha vikao ili kuona namna ya kushika madaraka,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

“Sio siri sana katika hili, watu wanahitaji nafasi mbalimbali iliwemo ya urais na wameunda mtandao mkali kabla ya kuanza kampeni zao,” kilisema chanzo cha taarifa hii.


Uongozi uliopo madarakani kikatiba unakaribia kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka mine.

No comments