MIRAJI ADAM AKACHA MECHI YA MAJARIBIO SINGIDA UNITED

BEKI wa zamani wa Simba, Miraji Adam amempiga chenga ya mwili kocha wa Singida United Hans Pluijim baada ya kushindwa kutokea katika majaribio ya kikosi, akihofia kuumia.

Miraji ambaye msimu uliopita alikuwa katika kikosi cha African Lyon kilichoshuka daraja Ligi Kuu Tanzania Bara, aligoma kufanyiwa majaribio ili baadae aweze kusajiliwa.

Akiongea jana, Katibu mkuu wa timu hiyo Abdulhaman Sima alisema mchezaji huyo alitakiwa kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Super Cup iliyomalizika juzi kwenda uwanja wa uhuru, lakini hakutokea.

Sima alisema kuwa kocha wao, Pluijim alitaka kumuangalia mchezaji huyo kwenye michuano hiyo ili kama akilidhishwa na kiwango chake waweze kumsajili na kushindwa kutokea kwake ni kama alikataa ofa yao.

“Miraji tulikuwa kwenye mazungumzo nae ya Ligi Kuu Bara na Koch alitaka amuone kwenye michuano ya Super Cup hakutokea tukaona kama alikataa,” alisema Sima.

Saluti5 ilimtafuta Miraji ili aweze kuzungumzia suala hili, akasema yeye ni mchezaji na alitoka kwenye Ligi kwa hiyo kiwango chake kinajulikana.

Miraji alisema, walichotaka Singida United kumfanyia majaribio kwenye michuano ya Super Cup ni jambo ambalo hakulitaka.


Alisema hakutaka kwenda kuichezea timu hiyo kwenye michuano hiyo kwa hofu ya kuumia wakati hana mkataba na klabu hiyo.

No comments