MKWASA AWAAMBIA WANA YANGA TULIENI USAJILI WA KISHINDO UNAKUJA

KATIBU mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Mkwasa amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki cha usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu bara na michuano ya kimataifa.

Katibu huyo alisema kuwa kuwakosa wachezaji wawili, Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar na jamal Mwambeleko wa Mbao FC sio mwisho wa Yanga kwa sababu bado wakati upon a ripoti ya kocha mkuu inafanyiwa kazi na Kamati ya Usajili.    
“Wanayanga wanapaswa kutulia kipindi hiki kwani bado kuna muda wa kutosha kufanyia kazi ripoti ya kocha, kwasababu dirisha la usajili ndio kwanza limefunguliwa Juni 15,” alisema Mkwasa.


“Hakuna haja ya kuvurugwa na habari za uhamisho zinazoendelea kwenye vyombo vya habari, Yanga ni klabu kubwa inajua inachofanya wakati huu, muda si mrefu kila kitu kitawekwa wazi,” alimaliza.

No comments