MKWASA: YANGA YA MSIMU HUU HATUTAKURUPUKA KWENYE USAJILI WA WACHEZAJI

KLABU ya Yanga imebainisha kwamba msimu huu haitafanya usajili kwa mhemko au kwa shinikizo bali itasajili kwa kutumia akili kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kikosi hicho.

Aidha katika usajili huo, Yanga itazingatia zaidi maoni na ushauri wa benchi la ufundi na si vinginevyo.

Kauli hiyo ni ya katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambaye ameamua kutolea ufafanuzi huo baada ya kuzagaa taarifa nyingi zisizo na mashiko kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

“Ninachoweza kusema ni kwamba usajili wa safari hii sio wa kukurupuka, tunajipanga na tunazingatia zaidi maoni na ushauri wa wataalamu wa benchi la ufundi maana wao ndio wanajua wanahitaji aina gani ya wachezaji,” amesema Mkwasa.

Aidha, Mkwasa amesema Yanga ina maeneo madogo tu ya kubadilisha na haihitaji kubadilisha timu nzima kama zinavyofanya timu nyingine.


Pamoja na hayo, Mkwasa amesema tayari wameshamalizana na wachezaji watatu wapya lakini kwa sasa wataendelea kufanya siri.

No comments