MNIGERIA OKOH HENRY TONY KUTUMIKA KAMA MBADALA WA VINCENT BOSSOU YANGA

BEKI mkongwe Vincent Bossou hana nafasi ya kuwepo katika kikosi cha Yanga msimu ujao lakini tayari Yanga imekaribia kumnasa beki kisiki raia wa Nigeria, Okoh Henry Tony.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba beki huyo anayecheza soka nchinmi Nigeria kwa sasa wakala wake yuko katika mazungumzo na uongozi wa Yanga tayari kwa ukamilisho wa uhamisho huo.

Beki huyo anayechezea Akwa United inayoshiriki Ligi Kuu Nigeria anatajwa kama beki kisiki anayejua kukaba kwa nguvu na kutopitika kwa kirahisi akitumia miguu yote miwili, huku urefu wake ukiwa ndio silaha muhimu.

Kocha wa Yanga katika ripoti yake ametaka asajiliwe beki wa kati mmoja mwenye uwezo wa kutumia mguu wa kushoto kutokana na kukosa beki mwenye uwezo huo katika mabeki wanaobaki katika timu hiyo.

Tayari mazungumzo na Yanga na wakala wa mchezaji huyo yanafanyika kwa siri chini ya katibu mkuu wa yanga Charles BonifaceMkwasa ingawa wakala huyo anataka beki wake asajiliwe mwaka mmoja kutokana na kuwa na mpango wa kwenda kucheza soka Ulaya.

“Tunazungumza nae, beki mzuri sana anajua kukaba vyema na ana mbinu nyingi za kukaba lakini pia ana utulivu mzuri na si mtu wa kucheza vibaya, kama tukikubaliana kila kitu tutamalizana nae,” alisema bosi huyo.


“Tunamalizia mazungumzo na wakala wake, lakini kama unavyojua usajili huu ni mapendekezo ya kocha wetu na baada ya kuona ugumu wa kumpata Yusuph Ndikumana sasa tunaona tumfuate huyu.”

No comments