MOHAMED SARAH ASEMA ANAJISIKIA FURAHA YA AJABU KUTUA LIVERPOOL

WINGA mpya wa Liverpool, Mohamed Salah amesema kwamba anajisikia furaha ya ajabu kutua katika wekundu hao.

Nyota huyo raia wa Misri amesema kuwa kujiunga kwake katika Liverpool kunampa nafasi ya kuonyesha tena thamani yake katika Ligi Kuu ya England.  

Amesema kwamba wapenzi wa Liverpool wanatakiwa kutegemea mambo makubwa zaidi kutoka kwake na kwamba anajua kuwa atakuwa Salah mpya kuliko wakati alivyokuwa na Chelsea.

Salah amewahakikishia mashabiki wa Liverpool kwamba yuko fiti kwa asilimia zote kuliko alivyokuwa anacheza akiwa Chelsea.

Nyota huyo amejiunga na Liverpool kwa uhamisho wa pauni mil 34.3 kutoka Roma ya Italia na anakuwa nyota mpya wa kwanza kusajiliwa katika kikosi cha kocha Jurgen Klopp kwenye msimu ujao.

Salah alionja utamu wa Ligi Kuu ya EPL akiwa na Chelsea kati ya mwaka 2014 na 2016 ambapo alicheza mechi 19 tu.

“Nimelipwa pesa nyingi kwa kazi moja tu. Kuonyesha thamani yangu na niwahakikishie wapenzi wa Liverpool kwamba niko fiti zaidi kuliko wakati mwingine wowote.”


“Kila wakati mambo yanabadilika. Nilikuwa mtoto sasa nimekuwa mkubwa, nilikuja England nikiwa kijana mdogo sasa nimekuwa na umri tofauti kabisa. Nina uzoefu wa kucheza katika timu tofauti. Nilikuwa Chelsea, Fiorentina na baadae Rom. Nimebadilika sana,” alisema.

No comments