Bosi wa Manchester United Jose Mourinho yupo tayari kumuuza mlinda mlango David de Gea kwenda Real Madrid kwa pauni milioni 22 tu, ila kwa sharti moja - apewe mshambuliaji Alavaro Morata.
Mourinho anamtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ili kuziba pengo la mkongwe Zlatan Ibrahimovic.
Morata anataka kuondoka Madrid na tayari amekuwa akiwindwa na vilabu kadhaa vikiwemo AC Millan na Chelsea.
Inaaminika United inataka pauni milioni 66 kwa De Gea, lakini ipo tayari kumtoa kwa pauni milioni 22 iwapo watapewa Morata aliyeifungia Real Madrid mabao 20 msimu huu licha ya kutokea benchi katika mechi nyingi.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac