MOURINHO AMUHAKIKISHIA NAMBA YA KUDUMU ALVARO MORATA MANCHESTER UNITED

Inadaiwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amempigia simu mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata aende Old Trafford na kumuhakikishia kwamba atakuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha United iwapo usajili wake wa pauni mil 60 utakamilika.

Mourinho amesema kwamba kiwango cha Morata ni kikubwa na anataka kuhamishia makali yake katika dimba la Old Trafford.

Amesema kuwa ingawaje kuna jitihada zinaendelea kusajili nyota wengine wakali akiwemo straika wa Torino ya Italia, Andrea Belotti, bado wanamtaka Morata.

Alvaro Morata ndie anayetajwa kurithi mikoba ya Zlatan Ibrahimovic ambaye anahusishwa na kucheza soka Uchina au Marekani.

Juzi Ijumaa Manchester United ilitangaza kwamba inatenga dau hilo la pauni mil 60 kwa ajili ya kumnasa Morata.
Dau hilo ni kubwa kuliko lile ambalo klabu ya AC Milan ya Italia imeweka mezani la pauni mil 39 ambalo ni kiasi kidogo.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja, thamani ya sasa ya Morata ni pauni mil 34 na alijiunga na Real Madrid msimu uliopita akitokea Juventus kwa thamani ya pauni mil 25.50.


Manchester United ndio wanaoweza kumnyakua straika huyo kwa sababu hawana uhakika kabisa wa kuwa na washambuliaji wake wawili, Ibrahimovic na Wayne Rooney.

No comments