MOURINHO AMWOMBEA "PO" PAUL POGBA KWA MASHABIKI WA MAN UNITED

KOCHA wa sasa wa Manchester United, Jose Mourinho amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwavumilia wanandinga waliomo kikosini msimu uliopita, akiwemo Paul Pogba.

Akinukuliwa baada ya United kupoteza mchezo dhidi ya Tottenham Hot Spurs, Mourinho alisema anakiangalia kikosi cha msimu ujao katika matumaini ya kufanya vizuri zaidi.

Huku akimtetea Pogba ambaye aliukosa mchezo huo kwa kufiwa na baba yake mzazi, Mourinho alisema wachezaji wote wa msimu huu ni wazuri hivyo mashabiki wawe na imani nao.

Pogba alisajiliwa na mashetani wekundu wa jiji la Manchester akitokea katika kikosi cha Juventus ya Italia.

Akinukuliwa na tovuti ya klabu ya United, kocha huyo raia wa Ureno alisema: “Ingawa bado hajaonyesha makeke yake ya kawaida lakini ninachoamini ana nafasi ya kung’ara mwanzoni mwa duru la pili.”

Awali, Mourinho amewahi kunukuliwa akisema alifanya uamuzi sahihi kumwita kundini Pogba na kwamba hatua yake hiyo itazaa matunda ifikapo mwishoni mwa msimu.


Aliyasema hayo baada ya kuwepo kwa lawama kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka wa ndani na nje ya England waliouponda usajili wa kiungo huyo kwa kile walichodai umetumia kiasi kikubwa cha fedha ambazo huenda hazilingani na mwanandinga huyo.

No comments